Teknolojia Mpya Yaanzishwa Kuvutia Kusoma Sayansi
KATIKA kuhakikisha wanafunzi wanalipenda somo la Sayansi, Taasisi ya Longitude Technologies wameanzisha program iitwayo ‘Stem Club’.
Program hiyo ambayo ni mpya nchini Tanzania, imeanza majaribio ya utafiti katika shule ya Mtakatifu Rosalia iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa progamu hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Musa Mishamo amesema lengo la kuanzisha program hiyo ni kuwavutia wanafunzi kuingia katika mambo ya sayansi na teknolojia kwa kufanya majaribio mbalimbali.
Amesema katika shule ya St. Rosalia wanafunzi takribani 400 watanufaika na program hiyo ya majaribio ambayo tayari imeonesha kufanya vizuri nchini Kenya kwa shule 1,000.
“Tunatumia vifaa mbalimbali ikiwemo Telescope kwaajili ya kuangalia anga moja kwa moja, tunaangalia mwezi sayari, nyota na jua na vitu mbalimbali vinavyoendelea katika anga.
“Pia kifaa kingine ni sehemu ambayo watu wanaweza kuingia na kujifunza masuala mbalimbali ya teknolojia na tunafundisha wanafunzi program ya kuttrack magari, pikipiki na kuongeza usalama katika jamii.
Published at HabariLeo