KilimanjaroPlanetarium

Longitude yaja na muarobaini somo la sayansi KilimanjaroPlanetarium

Longitude yaja na muarobaini somo la sayansi KilimanjaroPlanetarium

Katika kuhakikisha wanafunzi wanalipenda somo la sayansi, Taasisi ya Longitude Technologies wameanzisha program iitwayo ‘Stem Club’.

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha wanafunzi wanalipenda somo la sayansi, Taasisi ya Longitude Technologies wameanzisha program iitwayo ‘Stem Club’.

Program hiyo ambayo ni mpya nchini Tanzania, wameanzisha kama utafiti wa majaribio katika shule ya St. Rosalia jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa progamu hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi huyo, Musa Mishamo amesema lengo la kuanzisha programu hiyo ni kuwavutia wanafunzi kuingia katika mambo ya sayansi na teknolojia kwa kufanya majaribio mbalimbali.

Amesema katika shule ya St. Rosalia wanafunzi takribani 400 watanufaika na programu hiyo ya majaribio ambayo tayari imeonesha kufanya vizuri nchini Kenya kwa shule 1000.

“Tunatumia vifaa mbalimbali ikiwemo Telescope kwaajili ya kuangalia anga moja moja, tunaangalia mwezi sayari, nyota na jua na vitu mbalimbali vinavyoendelea katika anga. Pia kifaa kingine ni sehemu ambayo watu wanaweza kuingia na kujifunza mbalimbali ya teknolojia na tunafundisha wanafunzi program ya kuttrack magari, pikipiki na kuongeza usalama katika jamii.

“Lengo ni kuwafanya wanafunzi kwenda katika ulimwengu wa teknolojia kwa kuwaonyesha ambazo ziko nje ya nchi. Kwa Tanzania ni mara ya kwanza na tunaifanya kama somo la majaribio na badaye itasambazwa katika shule mbalimbali mijini na vijijini,” amesema Misamo.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa St Rosalia, Oscar Kondowe amesema wamefurahishwa na ujio wa program hiyo katika shule yao wanaamini itawasaidia wanafunzi wao katika masomo ya sayansi na kujifunza teknolojia.

Longitude yaja na muarobaini somo la sayansi KilimanjaroPlanetarium

“Tunajivunia kwa shule yetu kuwa ni shule ya kwanza kufanya majaribio ya program hii nchini, sisi walimu tutajitahidi maarifa tuliyoyapata hapa tuweze kuwaelekeza na wanafunzi wetu. Nimejifunza vitu vingi kama mwalimu wa sayansi hivyo naweza kuwaelekeza na watu wengine,” amesema Kondowe.

Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo, Leonard Daud amesema kuna faida katika kujifunza kwa vitendo kwani inasaidia kukumbuka kwa urahisi.

“Tunajiandaa na mitihani, kwa hiyo tunaposoma vitu kwa vitendo hata tunapokuwa tunajibu mitihani tunakuwa na uelewa zaidi na kuweza kufaulu mitihani yatu,” alisema Daud.

Naye Gabriella Deokary ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Rehoboth Christian School amesema amefurahi ni mara ya kwanza kuona Telescope, kwasababu shuleni wanaoneshwaga kwenye vitabu.

“Ninaona hii program ni nzuri kwa wanafunzi kwani tungeweza kuelewa zaidi tukiona vitu kama hivyo live kuliko kuona katika madaftari, ujio huu unaweza kuleta fursa mbalimbali kwa Tanzania,” alisema Gabriella.

Published By Tatu Mohamed Mwandishi, Mwananchi Communication Ltd (MCL)

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top